KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, April 17, 2014

UTEKETEZAJI WA BANGI KIJIJI CHA NGAOKOLA SONGEA VIJIJINI

 Asikari wa kikosi cha kuzuia ghasia akiwa amekaa katika shamba la bangi huko Magagula Songea Vijijini
 Majirani walioko katika mashamba ya bangi songea vijijini wakibadilishana mawazo na Asikari wa kikosi cha kuzuia ghasia
kazi ya kufika katika maeneo wanayo lima Bangi siyo Rahisi hapo Asikari wa Kikosi cha kuzuia ghasia akivuka katika madaraja mabovu yalioko Songea vijijini
 Mkongwe wa Habari Adamu Mzuza Nindi akiwa katikati ya shamba la bangi usitawi huo unatokana na pembejeo zinazo tolewa na serekari [VOCHA mkulima huyu akiwa amelima hekari moja na nusu Bangi hiyo ni kama unavyo iona
 Kamati ya ulinzi na Usalama ikiwa ina panda na kuteremuka katika Milima ya Ngaokola Songea Vijijini tayari kwa kwenda kuteketeza Bangi, Ukifika huwezi kuitambua sehemu inapo limwa pembeni kuna zunguka Mahindi au Ufuta
 Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Songea  ikiteketeza Bangi pamoja na Kung'oa Masalio ya Shina la Mti wa Bangi
 Ukisogea Hapo kama usipo jua kanuni za Bangi utajikuta umevuta bangi bila kutarajia baadhi ya watu walio kuwa hawajui kanuni za Bangi walijikuta Wakiwa wamelewa bila Kutarajia ,Unauona Moto huo ?
 Maeneo yaliyo pandwa Bangi kuna kuwa na Walinzi wa Jadi Unaye Mwona hapo ni Mbwa ambaye kazi yake ni kunusa harufu ya Mtu anaye karibia katika shamba la Bangi halafu hubweka kwa nguvu kuwa fahamisha walimaji Haramu wa Bangi kuwa kuna adui ana kuja Mbwa hao wako zaidi ya Sita
Katibu Tarafa wa  Mhukuru  Songea Vijijini Salima Mapunda akiwa ame beba Bangi tayari kwa kuteketeza

Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti amewataka Vijana kuacha kutumika kwa kazi haramu kama Kilimo cha Bangi ambacho kinaleta Madhara kwa watumiaji na hata kuwasababishia kuwa vichaa.
 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Songea (OCD) Alfred Kasoro amesema  walimaji wote wa Bangi orodha yake  anayo pia anajua  Viongozi wa Kisiasa wanaosimamia zoezi la  ulimaji wa Bangi. Pichani ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Songea Akongoza zoezi la kuing`oa Bangi katika kupambana na madawa ya kulevya.
 OCD Alfred Kasoro akionyesha mfabo wa kutofurahishwa na wale wote wanaoendelea na ulimaji au biashara ya Bangi amesema kampeni hii ya kuteketeza na kuwasaka wahusika wa shughuli hizi imezinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Songea itakuwa endelevu katika wilaya ya Songea.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akiteketeza shamba la Bangi lenye Ukubwa wa Ekari moja lililoko katika Kijiji cha Ngaokola Songea Vijijini Mkoani Ruvuma, amesema dhumuni la Serikali inapotoa vocha za kilimo ni kusaidia kuwainua wakulima wadogo ili waimarike kiuchumi lakini badala yake inashangaza kuona vocha hizo zikitumika katika kuimarisha Kilimo cha Bangi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Sixbert Valentino amesema amewaagiza watendaji wote katika Tarafa ya Mhukuru kukagua mashamba yanayotiliwa wasiwasi kwa Kilimo cha Bangi. Picha unayoiona ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri akishangaa jinsi bangi ilivyohudumiwa na kustawi vizuri.
Safari ya kuelekea Kijiji cha Ngaokola Songea Vijijini haikuwa rahisi kutokana na barabara na madaraja kuwa ya hatari kama unavyoona pichani Askari wa FFU wakitengeneza mazingira ya kusaidia gari kuvuka katika Daraja hiyo ya Miti.

No comments:

Post a Comment