KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, November 12, 2015

BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA (BAWACHA) MKOA WA RUVUMA WAMEMUOMBA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KUTENGUA UTAUZI WA ZUBEDA HASSAN SAKURU KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA RUVUMA


 Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ruvuma wamesema wanapinga vikali kuteuliwa Zubeda Hassan Sakuru kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
 Wanachama wa BAWACHA Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma wametoa Tamko la pamoja, wapo tayari kutoka CHADEMA endapo uteuzi huo hautabatilishwa  wamesema Zubeda Hassan Sakuru siyo mkaazi wa Mkoa wa Ruvuma hata wilaya waliyo sema ana toka Tunduru  hakuna hata mmoja anaye mjua . Jambo waliyo baini nikuona chama kipo mkononi mwa mtu mmoja.
 Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wakiwa ndani ya Ofisi za CHADEMA wilaya walipokutana kwa ajili ya kutoa tamko la kupinga Uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalum atakayewakilisha Mkoa wa Ruvuma uliofanywa na Uongozi wa CHADEMA Taifa.
 Wanawake wa CHADEMA kutoka wilaya za Tunduru, Nyasa, Mbinga, Namtumbo, Songea Vijijini na Songea Manispaa walipokutana katika Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea kutoa TAMKO hilo.
 wanachama wa Chadema wakiwa nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya Matarawe Manispaa ya Songea mara baada ya kutoa Tamko la Kupinga Uteuzi huo wa Mbunnge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.

Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wamemuomba Mwenyekiti wao wa CHADEMA Taifa Filiman Mbowe kubadilisha uteuzi alioufanya kumteua mtu ambaye hayuko katika Mkoa wa Ruvuma anaye tokea Tanga na kumteua kama mkazi wa Mkoa wa Ruvuma.
 Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma wameshangaa kuona hata Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma hawakuonekana katika kikao kilicho andaliwa rasimi kupinga uteuzi wa Zubeda Sakuru na kudai uteuzi huo wa kumfanya Mbunge wa mkoa wa Ruvuma wamedai umetumika kulipa fadhila zinazo tiliwa mashaka.
 Wanachama wa BAWACHA  nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea Mjini.
Wajumbe wa BAWACHA kutoka wilaya za Mkoa wa Ruvuma.

No comments:

Post a Comment