KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, November 19, 2015

UCHAGUZI WA KATA TATU NGAZI YA UDIWANI MKOANI RUVUMA WAKAMILIKA KWA CCM KUCHUKUA VITI VYOTE DHIDI YA CHAMA CHA CHADEMA

Mkurugenzi Mtendaji waq Halimashauri ya Wilaya ya Madaba Robert Mageni ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Madaba Songea Vijijini .Robert Mageni amekuwa Mahiri katika kusimamia uchaguzi kwa Jimbo hilo ukilinganisha na Majimbo Mengine ambayo amekuwa katika uzoefu. Lakini Jimbo la Madaba limeweza kufanya vizuri katika uchaguzi kuanzia ngazi ya Udiwani Hadi ngazi ya Ubunge na Uraisi
Uchaguzi katika Ngazi ya Udiwani katika Kata tatu za Mkoa wa Ruvuma Chama cha Mapinduzi CCM Kimeweza kuibuka Kidedea baada ya Kushinda Kata zote tatu.
Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Madaba na Jimbo la Namtumbo wamesema Kata ya Mkongo Gulioni na Kata ya Lismondi wa shindi  wote ni kutoka chama cha.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Namtumbo akiongea kwa njia ya simu akitoa Matokeo amesema Jimbo la Namtumbo lilikuwa na Kata 2 zilizofanya Uchaguzi kugombea udiwani mgombea wa CCM  Pandu Juma Alfani wa mkongo gulioni alimshinda mpinzani wake wa chadema Komba Dasitani Mcheshi kwa kura 1020 dhidi ya mpnzani wake wa CHADEMA aliye pata kura 222

Na kata ya Lisimondi mgombea wa CCM Athuman Likungwa aliweza kushinda mpinzani wake wa Chadema kwa kupata kura 762 dhidi Julius  Nyoni aliye pata kura 187
Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Udiwani wakiwa Makini kusoma majina ya walio jiandikisha ili uchaguzi usiwe na Mizengwe

Wananchi wa Kata za Mahanje na Mkongo Gulioni wameomba Viongozi walioshinda katika uchaguzi kuangalia changamoto za maji pamoja na Pembejeo za Kilimo.
Uchaguzi ulikuwa wa Uhuru na Haki huwezi kuamini huyo kijana yuko kijijini Madaba Songea Vijijini alkipiga  kura bila ya Hofu
Kanuni ya upigaji kura mara baada ya kupiga kura ili usirudie kupiga kura mara mbili hupakwa wino ambao haufutiki zaidi ya siku saba,wako walio taka kusafisha wino kwa nia mzuri tu ili kutoa uchafu ukiwauliza utasikia wakisema usijaribu ngoja utoke wenyewe
kiashirio kujua hiki ni kituo mabango yali bandikwa kila eneo la upigaji kura ili wapiga kura wasi hangaike
Mgombea kupiti tiketi ya chama cha Demokurasia na Maendeleo CHADEMA Kata ya Mahanje Hans John MLelwa ambaye alipata kura 487  Na ndugu Mgombea wa CCM Ndugu Stephano Nelson Mahundi kuwa Mshindi wa Udiwani baada ya kupata kura 946 
                                             Kuhakiki Majina mara kwa mara ili kuwa ndiyo kazi kubwa
Mpiga kura akipewa karatasi ya kupigia kura katika kata ya Mahanje songea Vijijini
Popote unapo kwenda kibao ni moja ya ishara kujua kuko sehemu gani ukisoma uta jua kuwa Tanzania ina alama ya kujua hapa ni wapi na una elekea wapi
Kazi ya Uchaguzi siyo mdogo wasimamizi walifanya kazi Mpaka usiku ili kufanikisha uchaguzi ngazi za Udiwani
Ulinzi katika uchaguzi ni Mhimu lakini kutokana na Amani tuliyo nayo Watanzania Asikari wame kakaa kwa Amani huku wanchi wakipiga kura bila fujo wala Bugudha
Kazi ya kujumulisha Matokeo ilikuwa kazi kubwa hasa kwa kufanya kazi kwa kutumia Taa lakini wasimamizi hawa kuweza kuchoka mpaka alipo tangazwa mshindi
Mweka Hazina na Mkurugenzi Mtendaji wakijadili jinsi ya kuwezesha watu walio shiriki kusimamia uchaguzi ukizingatia kuwa Uchaguzi huu ulifanika Vijijini ambako baadhi ya Huduma ni finyu lakini Mkurugenzi Mtendaji aliweza Kumudu
Aliye kaa katikati ni Ndugu Fungo na kulia kwake ni Msimamizi mkuu wa uchaguzi ndugu Robert Mageni na aliye kaa kushoto ni Mweka hazina Halimashauri ya Madaba

Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Mahanje Jimbo la Madaba  Kanisius Lingowe amemtangaza Mgombea wa CCM Ndugu Stephano Nelson Mahundi kuwa Mshindi wa Udiwani baada ya kupata kura 946 dhidi ya Mpinzani wake wa CHADEMA ndugu Hans John MLelwa ambaye alipata kura 487
Aliye simama wapili kutoka kushoto ni ndugu Mlelwa aliye shinda kiti cha udiwani kata ya Mahanje
Msimamizi wa jimbo la Madaba Robert Mageni aliye vaa tisheti ya punda milia aki wauliza walivyo ona uchaguzi na kuwauliza kama kuna tatizo lakini hakuna aliye toa kasoro
Uchaguzi ni uchaguzi kuwa makini ni moja ya sifa ya wasimamizi unaona jinsi wasimamizi wanavyo hakiki majina ili kila chama kilidhikje na uchaguzi au mutu atakaye teuliwa


Mkoa wa Ruvuma wenye Majimbo 10 ya Uchaguzi,  CCM imeweza kutwaa Mjimbo yote ikiwa na pamoja na kuongoza halimashari zote kiutendaji

No comments:

Post a Comment