KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, November 17, 2015

WAAATHIRIKA WA MAAFA YA KUEZULIWA NYUMBA ZAO MANSPAA YA SONGEA WAPATA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI


 
Serikali Wilayani Songea  Ruvuma imetoa pole kwa Wananchi waliopatwa na
Maafa baada ya Nyumba zao kuezuliwa na Upepo ulioambatana na Mvua kali
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya amesema Kamati ya Maafa Wilaya ya Songea baada ya kuona hali  mbaya ya Kaya 8 aliona ni  bora ianze na kaya hizo, akitoa msaada huo alieleza nia ya serikali  kwa wananchi wake wakati akimkabidhi bati  Christina Kambanga wa Mtaa wa Namanyigu Kata ya mshangano.

 Mhandisi wa Ujenzi Manispaa ya Songea akihakiki Bati wakati wa kukabidhi kwa waathiriwa walioezuliwa nyumba zao.
 Kamati ya Maafa Wilaya ya Songea imeweza kukabiliana na Janga la kueziliwa kwa nyumba za baadhi ya wananchi wake kwa kutoa Msaada kwa kaya 8 ukiwa na Thamani ya Shilingi 1,050,000.
 Baadhi ya Nyumba zilizoezuliwa Kata ya Mletele Manispaa ya Songea, kama inavyoonekana bati zikiwa zimetupwa mbali na upepo ulioambatana na mvua iliyonyesha tar 1/11/2015

 Kama inavyoshuhudia nyumba ikiwa imeezuliwa paa katika Eneo la Mtaa wa Unangwa kata ya Seed Farm Manispaa ya Songea.
 Nyumba ikiwa ilivyoezuliwa paa Kata ya Seed Farm.
Wananchi waliopata Msaada huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Unangwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Maiko
Mpangala amesema kauli ya mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr.
 John Pombe Magufuli ya kusema hapa kazi tu, imethibitika baada ya wananchi kupatwa
na janga la kuezuliwa nyumba zao,k iliyoungwa mkono na waliopatwa na
Maafa hayo.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya akieleza Hali halisi ya Uharibifu huo, na kuainisha gharama ya msaada uliotolewa na Kamati ya Maafa
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya amesema mara nyingi jamii inapopatwa na janga inakuwa haina jinsi ya kufanya ila hukabilianana janga hilo kwa kuchangishana baadhi ya garama ama huishia kukata tamaa.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya akitoa pole  amesema Manispaa yaSongea  imepatwa na  Janga hilo ambapo Nyumba zaidi ya 15 zimeezuliwa.

No comments:

Post a Comment