KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, November 16, 2015

NFRA MKOA WA RUVUMA YA ELEMEWA NA MZIGO WA MAHINDI ,WALIO PEWA VIBALI WAOMBA KUJA KUCHUKUA MAHINDI HARAKA



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ameiomba Mikoa ambayo imepata kibali cha kuchukua Mahindi katika Hifadhi ya Chakula NFRA  Mkoa wa        Ruvuma waje haraka ili kupunguza wingi wa Mrundikano wa Mahindi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema Hifadhi ya Chakula ya Mkoa wa Ruvuma ina Tani zaidi ya Laki Moja, kutokana na hali ya Masika inayokuja Mahindi yanaweza kuharibika.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema kutokana na Mlundikano uliopo wa Mahindi katika ghala la kuhifadhia mahindi  NFRA kuwa mengi. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameiomba Mikoa iliyo pata kibali cha kuja kuchukua Mahindi waje haraka ili  kutoa nafasi ya kuweza kupokea Mahindi mengine kutoka kwa wakulima
Mkuu wa Mkoa amesema Mwaka huu serekari haikopi mahindi ya Mkulima ina nunua kwa Fedha Tasilimu


Wakulima kuuziwa Pembejeo feki kwa kuwekewa Chumvi na Simenti ni njia moja wapo ya kurudisha maendeleo ya wakulima ukizingatia Mkulima wa Tanzania hana Bima hata akikosa Mazao Shambani hilo lina kuwa swala lake Mwenyewe

 Vijana wakijitahidi kupakia Mahindi ili kupeleka Sehemu ambako hakuna Chakula lakini hata Hivyo haionekane palipo chukuliwa Mahindi

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amewaonya wale wote wanaouza Pembejeo  feki kwa kuwadanganya wakulima  kuwa ni Mbolea kumbe wametia Chumvi au simenti, Watu hao wakikamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

 Meneja wa NFRA Mogani akiongoza msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akionyesha hali halisi ya Mlundikano wa Mahindi katika Ghala la NFRA
Kama unavyo ona mahindi yalivyo Rundikana yana hitaji kuondolewa ili nafasi ya kuweka mahindi mengine, kuna zaidi ya tani laki moja hivyo Mikoa yenye njaa au iliyo pewa kibali ije kuchukua Mahindi

No comments:

Post a Comment