KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, November 22, 2015

MTAZAMO WAWANANCHI KWA RAIS WA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA DR JOHN POMBE MAGUFULI UKOJE

Mungu ndiye mwanzilishi wa kuchagua Viongozi, tunaambiwa mtu wa kwanza aliyetawala Dunia alikuwa Adamu. Utawala wa Adamu ulikuwa wa huruma, Ukatili ulianza pale mtoto wa Adamu  Kaini alipomuua Habil.      Hivyo hivo tunaona Utawala wa Yusufu alikuwa mdogo na nduguze waliamua kumuuza mdogo wao lakini ndiye aliyewaokoa wakati wa njaa.                                                                                                                                                     Hebu tuone Daudi naye alikuwa mtoto mdogo kazi yake kazi yake kubwa ilikuwa kuchunga lakini Mungu alipotaka kuweka mtawala aliamua kumteua Daudi.                                                                                                             Sasa ninachotaka kusema ni jinsi gani Mungu ameweza Kumteua Dr. John Pombe Magufuli kuwa Rais, ni mfano wa Manabii waliopita,  kazi ya Mcha Mungu kuwaonea  huruma watu wanaoteseka. Hata Yesu alipofika Hekaluni alikuta Mafarisayo wakifanya Hekalu la mungu kuwa Soko. Lakini alimwaga vitu vyote na alisema msifanye Nyumba ya Mungu kuwa Soko la Wanyang`anyi.                                                                                              
Hivyo hivyo Rais Magufuli wakati wa kumwapisha Waziri Mkuu Majaliwa Kasim, watu walichanga fedha shilingi milioni 225 ili wafanye Sherehe lakini Rais akaamua kuzipeleka Fedha hizo katika Hospitali ya Taifa ya muhimbili na kuwezesha kununua Vitanda, Magodoro pamoja na shuka, suala kama hilo linahitaji ujasiri.

Hotuba yake aliyoitoa katika Bunge la 11 ameeleza jinsi fedha za Serikali zilivyokuwa zinashindwa kutumika ipasavyo kwa wanyonge, ambapo fedha nyingi zilitumika pasipokujali matatizo ya watanzania. Fedha zilizotumika kwa safari za nje zingeweza kufanya mambo makubwa.

Sasa jee? Mtu katoka CCM ni mchaguliwa wa CCM waliokuwa wanafuja fedha ni viongozi hao  hao wa CCM. Anapowafichua Mafisadi, wala Rushwa tegemeo lake ni nini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hivi sasa anasali sala ya Yesu Msalabani akisema Eloi, Eloi Lamasabakisani, Mungu wangu Mungu wangu kwa nini unaniacha.

Watanzania tujue kuwa Sala hiyo ni sawa wanavyosema Waislamu Ihidina Sita la Mstakimu Silataladhina  Ana mnta wala dhuarimu ghairimu maudhubi wala dhuarimu. Utuongoze katika njia ya watu walionyooka na sio wale walio wakasirikia.

Ndugu zangu, ninachomaanisha Mtu akiomba msaada hatuna budi kumsaidia, Rais wetu anataka silaha kali ya kumsaidia. Vita hii sisi Watanzania wote tuingie madukani kununua Bunduki kuwa Askari wa Rais Mteule wa Awamu ya Tano Dr. John Pombe Magufuli.

Silaha zinazotakiwa ni mkristo kununua Biblia na kuomba kwa Bidii, na Muislamu kununua Kurani Tukufu na kusimamisha sala tano ili Rais afanikiwe katika Vita hii.

Viongozi wanaojitoa kwa moyo wote wanatakiwa kusaidiwa, Miaka zaidi ya 51 iliyopita tulikuwa tukiomba kumpata Rais atakayewasaidia wanyonge, Siku ya kwanza Muhimbili alitoa Pochi yake kutaka kumlipia Bili ya Matibabu Mgonjwa. Jee, hapo huoni kuwa hali hizo zinamkera?

                                                                                                                                                                           
               


 Adam Nindi mkurugenzi wa Blog ya Songea Habri akiwa na Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli, hii ina maanisha viongozi wa juu walivyokuwa karibu na wananchi wote hata wadogo.
 Rais awamu ya tano Dr. John pombe Magufuli kipenzi cha watanzania akishukuru kwa kumuamini kuongoza watanzani na kuwathibitishia kuwa kwake ni kazi tu.

Rais wa Awamu ya nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amejitahidi kuiongoza Nchi mpaka kufikia hali hii tuliyokuwa nayo, Ni nadra kiongozi anayetawala kuweza kukabidhi utawala kwa Amani.   Kwa wastani hakuna mtu asiyekosea isipokuwa Mungu, Maksi ya Dr Jakaya Mrisho Kikwete ni kule kusimamia Amani na Utulivu na ndicho kilio cha Walimwengu wote.


Picha ya hapo juu ni picha inayoonyesha jinsi waandishi walivyokuwa wakiwajibika kutangaza habari za kuweza kuiweka Nchi yetu katika Amani ili Uchaguzi uwe wa Haki na uhuru. Adam Nindi M

 Watanzania ni watu waliokuwa na msimamo wa kuendeleza na kuilinda Amani na utulivu kama inavyojieleza nembo hiyo hapo juu.
Rais Mteule wa Awamu ya Tano alikuwa akitoa mfano wa wazi kuhusu Maendeleo ya Tanzania, alisema barabara za lami zimejengwa wale ambao hawana magari wasingelijua hilo, akitoa mfano mdogo kuwa katika simu unampigia mpenzi wako I Lovw You; hayo ni maendeleo ukilinganisaha na wakati wa TTCL Unakaa foleni mpaka uipate laini kumekucha, hapo Rais akipiga Simu.

Picha iliyo mbele yako ni Adam Nindi akisalimiana na Rais wa awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa, hiyo ni ishara ya kuwa Viongozi wa Tanzania wanawajali watu wadogo,  Adam Nindi na Rais Mkapa wapi na wapi lakini huo wote ni upendo.


Adam Nindi akimuuliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Madini yaliyopo Mkoa wa Ruvuma, Watanzania watafaidika vipi kwa kuwa Mikoa yenye Madini mara zote watu wake wanakuwa wa kwanza kufaidika.


Adam Nindi akiwa na Rais Karume wa  Zanzibar akimuuliza akiuliza jinsi gain atakavyosimamia Muungano wa Zanzibar baada ya kuona watu wachache wakiubeza Muungano, lakini Rais Karume alikuwa imara aliongoza vizuri na mpaka anatoka Muungano ameuacha imara.

No comments:

Post a Comment