KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, November 19, 2015

WAZEE WALALAMIKA KUTO PEWA RISITI WANAPO FANYIWA OPARESHENI KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA


Wazee Mkoani Ruvuma wameulalamikio Uongozi wa hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa kushindwa kupewa risiti mara wanapofanyiwa upasoaji na kutoa Fedha.

Wazee hao wakiwa katika Semina iliyoshirikisha Wauguzi na Madaktari wa Mkoa wa Ruvuma katika Ukumbi wa Unangwa Manispaa ya Songea wamesema pamoja na wazee kutakiwa kutibiwa bure wanapofanyiwa upasuaji wanalazimika kutoa Fedha lakini hawapati risiti.

Mzee Khamisi Mandilu amesema anao ushahidi wa Wazee wawili ambao walifanyiwa upasuaji lakini hawakuweza kupewa risiti, jambo jingine ni lugha za matusi ambazo hupewa wazee

Madaktari wamesema kila Zahanati au Hospitali inatakiwa kuwa na Dirisha la Wazee na ikiwezekana kila Zahanati iwe na Kitengo Maalumu cha kutoa Huduma kwa Wazee.

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea amesema wazee wanatakiwa kupewa elimu ya mara kwa mara ili likitokea jambo wawe na mtu wa kuweza kuwakilisha changamoto zao badala ya kusubiri mpaka linapotokea jambo

Wauguzi nao wameitaka jamii kuwa karibu na Serikali badala ya kungoja kila huduma ya Wazee ilipwe na Serikali

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Gumbiro Ugezedu Beda amesema Wazee ambao hawana Bima ya Afya ili kuepukana na masuala ya kuambiwa hakuna Dawa akilipia Bima ya Afya basi ataweza kupata huduma bure.

Mwandishi wa Star TV na RFA Songea Bw. Adam Mzuza Nindi akiandaa habari juu ya Changamoto zinazowakabili wazee katika Ukumbi wa Unangwa Manispaa ya Songea ambako semina ya kujadili changamoto za wazee imefanyika chini ya Shirika la PADI.
Adam M. Nindi Mmiliki wa Blog ya Songea habari andaa taarifa katika semina iliyowakutanisha wazee, wataalam wa Afya na Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea na Manispaa kujadili mustakabali wa changamoto zinazowakabili wazee.
Wazee pia wameiomba Serikali kuwatengea madaktari maalum wa magonjwa ya wazee kama ilivyo kwa akina mama na watoto ambao wana madaktari wao maalum waliosomea magonjwa ya akina mama na watoto.
Semina ya Wazee na Wahudumu wa Afya ambayo imeandaliwa na Shirika la PADi Shirika linalohudumia Wazee Mkoani Ruvuma imeazimia kuwa na Mikutano ya mara kwa mara ili kujua changamoto zinazowakabili wazee.

1 comment:

  1. Tunapenda sana wakati mwingine penda kutuwekea stori za tukio zima na picha zake kuliko muda mwingi kujaza picha bila stori. Tutajuaje nini kilikuwa kikiendelea huko bila stori mwandishi unayejiita mkongwe wa habari?

    ReplyDelete