KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, November 27, 2015

WAFANYABIASHARA MKOA WA RUVUMA WATOA MCHANGO WA BATI KWA MKUU WA WILAYA YA SONGEA ILI KUWAPA WAHANGA WALIO EZULIWA NYUMBA ZAO


Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya amesema Serikali inawathamini wafanya Biashara wanaoungana na Serikali katika kutatua Matatizo  ya wananchi kuwa ni wafanya Biashara  werevu.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya amewataka wafanya biashara wajue kuwa Serikali inatambua kuwepo kwa wafanya biashara hasa pale wanapoungana na serikali kuwasaidia Wananchi wanapopatwa na Majanga.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya ameyasema hayo alipokuwa akipokea bati 112 na misumari ya bati kutoka kwa wafanya biashara wa manispaa ya Songea kwa lengo la kuwasidia wananchi walioezuliwa Nyumba zao na upepo mkali ulioambatana na mvua na kuziacha familia 15 bila kuwa na mahali pa kulala.

 Mkuu wa Wilaya ya Songea akielekeza jinsi yakuimarisha nyumba kabla ya kuezeka amesema haraka haraka au mtu kutaka nafuu ndicho chanzo cha nyumba kuezekwa tofauti. Amesisitiza kuwatumia wahandisi kabla ya kuezeka ,Wahandisi hulipwa Mshahara kwa ajili ya kuwasaidia wananchi elimu waliyonayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea akipewa Maagizo na Mkuu wa Wilaya jinsi ya Kuwa saidia watu wanao ishi pembezoni ili waweze kuepukana na Majanga, amesema njia moja wapo ni kuwatembelea mara kwa mara na kuona kazi za maendeleo wanazozifanya zifanyiwe marekebisho kabla ya Madhara kutokea.

Mwenyekiti wa Wafanya Biashara Mkoa wa Ruvuma Issack Mbilinyi (Mwilamba) amesema wafanya biashara ni moja ya Jamii, hawawezi kuona watu wanateseka na wao wana pesa wakashindwa kusaidia Jamii bora ni ile inayosaidiwa katika Matatizo.

 Watu wa kijiji cha Nakahegwa wakichukua bati za msaada walizo letewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hlimashauri ya Wilaya ya Songea Sixbet Valentin akiwa na Kaimu Mkurugenzi Weniselia Swai wakibadilishana mawazo ya kuweza kuimarisha uchumi pamoja na kuangalia upandishaji wa mazao ya biashara kama Mahindi,Kahawa na Maharage.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nakahegwa Songea Vijijini Damiani Sanga akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Beson Mpesya na kutoa shukurani kwa msaada wa Bati walio pewa wananchi wake
Wahanga waliopatwa na Matatizo ya kuezuliwa Nyumba zao katika Kijiji cha Nakahegwa waligala gala chini kushukuru kwa msaada waliopewa na kusema kweli huu ni Utawala wa sasa kazi
 Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya akiwa na familia ya Mzee Golihama wahanga wa kuezuliwa nyumba zao huko katika kijiji cha Nakahewgwa Songea Vijijini. kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Sixbet Valentine na katikati ni wahanga walioezuliwa nyumba zao Bibi Maria njovu na kijana wake John Matias Goliama.
 Kiongozi bora ni yule anayepaswa kufuatilia kwa karibu matatizo ya wananchi wake anaowaongoza na kushiriki katika kuyatatua. Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Sixbert Valentine akiwa na watoto wa wazazi waliopatwa na maafa ya kuezuliwa nyumba zao kwa mvua iliyoambatana na upepo katika Kijiji cha Nakahegwa Songea Vijijini ambapo mkurugenzi aliwapa kiasi cha fedha ili wanunue daftari za shule kufidia daftari zilizoharibika kwa kunyeshewa na mvua.

Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa ambao unapata Mvua nyingi zinazoambatana na upepo mkali, Mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya amewataka wahandisi wa serekari Songea kutembelea wananchi na kuwaelekeza jinsi ya kulinda nyumba zao na upepo kwakufunga Tengo zinazozuia upepo badala ya kuwaacha wakizuia upepo kwa kufunga nyaya za matairi ya Magari.

 Baadhi ya nyumba zilizopatwa na maafa ya kuezuliwa na upepo ulioambatana na mvua katika kijiji cha Nakahegwa kata ya mbinga Mwalule Songea Vijijini.
Uongozi ni utumishi, kitendo cha mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya na kamati yake ya Maafa wilaya kubuni mbinu ya kukusanya michango kwa ajili ya kwenda kuwafariji wahanga walioezuliwa nyumba zao kupitia wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wafanya biashara waliopo katika eneo lake ni tendo la faraja kwa wananchi ambalo linastahili kuigwa kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea kusubiri mfuko maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu.

No comments:

Post a Comment