KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, February 20, 2016

BENK YA POSTA NCHINI TANZANIA YA KARABATI VYOO VYA SHULE YA MSINGI MAKAMBI SONGEA


Shule ya Msingi ya Makambi Manispaa ya Songea yenye Wanafunzi 850 imepata ufadhili wa kukarabatiwa kwa vyoo vyenye Matundu 12 vikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 4.7
Afisa Mahusiano wa Benki ya Posta Noves Mosses amekabidhi vyoo hivyo  kwa Mwalimu Msaidizi  Kanisius Ngongi baada ya Uongozi huo kuomba ufadhili wa kukarabatiwa vyoo vitakavyo tumika  kwa Watoto  850 ambao walikuwa wakitumia vyoo hatarishi  

Afisa Uhusiano wa Benk ya Posta Noves Mosses ameitaka jamii kuwa na imani na Benki ya Posta kwa kutoa ushirikiano na Benki ya posta . pia amemeomba tasisi nyingine za kifedha kuji kita katika kuisaidia jamii kwa  kutatua changamoto zinazo wakabili kama  Elimu Afya na Shuguli zingine za kuleta maendeleo kwa jamii.

Mwalimu wa  Shule ya msingi Makambi Jeni Lugongo akimwakilisha mwalimu mkuu  ameomba Wafadhili mbalimbali wakiwemo Benki ya posta kuwasaidia walimu  kukarabati  choo  cha walimu ili kiendane na hadhi zao kama walivyo fanya kwa wanafunzi
Afisa Uhusiano wa Benki ya Posta nchini Tanzania Noves Mosses   amesema nia ya  Benki  ya Posta kazi yake ni kuunga mkono juhudi za serekari katika  kutatua changamoto za  sekita ya elimu ,Afya na Ustawi wa Jamii  Benk ya Posta imekuwa ikisaidia jamii kwa kujenga Madarasa,Kutoa Madawati na sasa imeweza kukarabati vyoo vya Shule ya Msingi Makambi
Afisa uhusiano wa Benk ya Posta Noves Moses akibadilishana mawazo na walimu huku akiwa elezea faida ya kujiunga na Benk ya Posta .kwanza kuwa na uhakika wa kukopo na kufanya shuguli za kusaidia familia mojamoja pili kufungua Acount ya watoto kwa ajili ya Elimu hivyo ni juu ya kila mwalimu kuonyesha mfano wa kufungua Acount Benk ya Posta

Wanafunzi wa Shule ya msingi Makambi Manspaa ya Songea  wamesema wana ishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kukarabati vyoo kwani hapo awali Wanafunzi wote bila kujali jinsia walikuwa wakitumia choo kimoja  Jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa watoto wa kike kuweza kupata magonjwa ya kuambukiza. Wameomba  Tasisi za kifedha  zingine  kuiga mfano huo
 Wanafunzi wa shule ya msingi makambi manspaa ya songea wa kifurahia kupata vyoo vya kisasa

Benki ya Posta katika Mkoa wa Ruvuma imekuwa mstari wa mbele kuchangia upande wa elimu tayari ilishatoa Madawati 50 kwa  Shule ya Msingi Mbulani Kata ya Ruvuma na kutoa zawadi kwa Wanafunzi waliofaulu kwa kupata Division One katika shule  za mkoa wa Ruvuma.  

No comments:

Post a Comment