KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, February 21, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA YA GHAFLA MKOANI RUVUMANaibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala amesema hata hospitali ya Mkoa wa Njombe am,bayo ilikuwa inakusanya shilingi  Milioni 3 kwa mwezi sasa inakusanya shilingi milioni 15 pamoja na mapungufu yaliyojionyesha ambayo kama hawatayarekebisha kwa  muda wa miezi mitatu Hospitali hiyo itaweza kufungiwa.Naibu Waziri wa Afya akiongeza kuhusu Madai ya Watumishi wa Sekta ya Afya, amesema Serikali inajipanga kulipa Madeni hayo imeanza Mwezi Januari Mwaka huu na itaendelea kuwalipa Watumishi wote wanaodai stahiki zao.Ziara ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr. Kigwangala ni ya kushitukiza ameweza kutembelea wodi ya watoto, Maabara na sehemu ya Upasuaji na kukuta changamoto ya baadhi ya Mashine za maabara zikiwa mbovu na Sehemu ya Upasuaji Vitanda vikiwa vimepitwa na wakati. Akielezea kuhusu mafanikio ya kutumia mfumo wa Mashine za ELECTRONIC katika Hospitali ya Rufaa ya Mhimbili asema  mapato yame ongezeka mara mbili kuliko mwanzoPia amezipongeza Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma na Hospitali ya Mjimwema kwa  kuweza kuboresha Huduma za Mama na Mtoto.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya amesema Hospitali ya Mkoa hivi sasa baada ya kufunga Mashine za ukusanyaji mapato za ki electroniki imeweza kuongeza Makusanyo  kutoka shilingi milioni moja laki mbili hadi kufikia milioni 60 kwa mwezi   , Naye Mganga Mkuu wa hosptali ya Mkoa amesema Vifo vya Mama na Mtoto sasa vimepungua kila wanawake 100,000 vifo 95 tu vinavyotokea.

NAIBU WAZIRI WA AFYA JINSIA WAZEE NA WATOTO  DR. HAMISI  KIGWANGALA AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA NA KITUO CHA AFYA CHA MJIMWEMA NA KUKUTA CHANGAMOTO YA BAADHI YA MASHINE ZA MAABARA MBOVU NA BAADHI YA VITANDA VIBOVU KATK CHUMBA CHA UPASUAJI.

Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala ameyasema hayo katika ziara ya kusitukiza mkoani Ruvuma alipo tembelea Hospitali ya songea na Hospitali ya mji mwema Manspaa ya songea

Naibu Waziri wa Afya Jinsia Wazee na Watoto Dr Hamisi Kigwangala amesema ukusanyaji wa Mapato kwa kutumia Mfumo wa Electronic umeweza kuongeza Mapato katika Maeneo yote ya hospitali zinazotumia mfumo wa Mashine za ELECTRONIC
Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala amesema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hapo awali ilikuwa inakusanya Mapato kwa kupata Bilioni 2 milini 700    kwa sasa inapata Bilioni 4 milini 400    kwa mwezi. Jambo ambalo linaweza kupunguza Changamoto zinazowakabili watumishi kwa kulipa Madeni ya Malimbikizi ya madeni wanayodai.


Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala amesema hata hospitali ya Mkoa wa Njombe am,bayo ilikuwa inakusanya shilingi  Milioni 3 kwa mwezi sasa inakusanya shilingi milioni 15 pamoja na mapungufu yaliyojionyesha ambayo kama hawatayarekebisha kwa  muda wa miezi mitatu Hospitali hiyo itaweza kufungiwa.

No comments:

Post a Comment