KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, August 25, 2013

POLICE SONGEA WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA RUVUMA


Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa  kukabiliana na Vitendoi vya Unyanyasaji wa Kijinsia Mpaka sasa kesi zaidi ya 400 katika kipindi cha 2012/2013 zime weza  kuwabainika ,Na  wanawake 6 waliobakwa na kuuwawa kesi zao ziko Mahakamani . Kubwa zaidi  Police Wanawake wamefanikisha kujenga  Jengo la polisi Wanawake lililogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 30 ambalo  mpaka sasahalijaanza kazi  kutokana na kukosekana kwa Milango na Madirisha.

 Mtandao wa police wanawake Mkoa wa Ruvuma kila wakati wamekuwa wakijitolea kuona wagonjwa na kuwafariji wanasema huo ndio moyo wa mwanamke aliye zaliwa na Mwanamke mwenye Huruma
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma umewataka wanawake kuachana na vitendo vya kikatili kwa kutoa adhabu kali kwa Watoto pale wanapokosea. Pia kuachana na tabia ya kutelekeza Watoto na wengine kuwauwa.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo ameyasema hayo wakati wa kuadhimisha Wiki ya Polisi Wanawake ambayo iliongozana na kutoa zawadi kwa wagonjwa 250 wakiwemo Wanawake waliojifungua 85 na Wanaume waliolazwa Hospitali ya Mkoa.


Naye Msimamizi wa Dawati la Polisi Wanawake wilaya ya Songea Mrakibu Msaidizi wa Polisi Paulo Mashimbe amewataka wan aume nao kujitokeza katika kubanisha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na Wanawake.

 Wagonjwa Mbalimbali walipata zawadimbalimbali ikiwemo matunda,nguo,na sabuni za kufulia
 WP Police wakike akionyesha mapenzi kwa mtoto aliyoko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
 Mtoto akionyesha furaha baada ya kutembelewa na Mtandao wa Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma


Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  Walta Soko amesema Wanawake wameumbwa kwa Roho ya kuwa na huruma, wanawake waache kuiga tabia ya kuwa wakatili huko ni kukosa  Maadili halisi ya wanawake.
Naye Muuguzi wa Wodi ya Wazazi ya Wanawake amesema Tendo la Polisi Wanawake kutoa Msaada ni tendo lenye fundisho kwa Wazazi wote wa Kike na wa Kiume

No comments:

Post a Comment