KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, August 14, 2013

WATU WAO ISHI PEMBEZONI HUWA WAKWANZA KUFAIDI MATUNDA YA WAGENI KUTOKA NJE NDIVYO ILIVYO KWA WATU WA LITISHA Wasanii wa Ngoma ya Asili ya Kinyasa ijulikanayo kwa jina la Mganda wakitumbuiza katika Sherehe ya Jubilei ya Miaka 25 ya Huduma ya Afya ya Msingi iliyofanyika katika Kijiji cha Litisha Peramiho Songea Vijijini.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho Dr. Ansgar Stuffe (kushoto) akiwa na wageni wake kutoka Ujerumani Rais wa Benki ya Ujerumani Frant Mader na Binti yake Franz Mader wakikagua mabanda ya utekelezaji wa shughuli za Afya ya Msingi zinazosimamiwa na Dr. Ansgar Stuffe katika kuboresha Afya za Jamii iliyo pembezoni.
 Dr Ansgar Stuffe akiwa na wananchi wa Kata ya Ruvuma katika kusherekea jubilei ya Miaka 25 ya Utekelezaji wa Huduma ya Afya ya Msingi kwa wakazi wa Tarafa ya Ruvuma Peramiho Songea Vijijini
Ngoma ya Mganda ikishirikisha wanawake hebu ona wanawake wanavyo sakata ngoma , hii ni kuonyesha Wanawake wanaweza
 Wahudumu wa Afya Vijijini (WAVI) wakifurahia Mafanikio ya Mradi wa Afya ya Msingi katika kipindi cha miaka 25, 1988 - 2013 kwa wananchi waishio pembezoni kata ya Ruvuma wilayani Songea Vijijini. Juhudi hizo zinatokana na jitihada za Dr. Ansgar kwa kushirikiana na Wahudumu wa Afya katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa yakiisumbua jamii hiyo.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho na Mfadhili wa Mradi wa Huduma ya Afya ya Msingi Vijijini akikagua Mabanda ya Maonyesho ya namna ya kujikinga na Afya Bora katika kuadhinisha jubilei ya Miaka 25 ya Utekelezaji wa Huduma hiyo kwa kuboresha huduma ya maji, kinga ya Malaria kwa kuwapa chandarua na kutokomeza magonjwa yaliyosahaulika.

No comments:

Post a Comment