KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 29, 2012

APIGWA MSHALE NA KUFA PAPO HAPO -SERENGETI

MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHARE,


Na Anthony Mayunga-Serengeti.

Oktoba 27,2012.

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe kata ya
Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas
Wambura(17)anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani
Chacha Damiani Mangali(18) na kufa papo hapo.

Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26,majira ya saa 2 mwaka huu
usiku nyumbani kwa marehemu Mangali limethibitishwa na uongozi wa
kitongoji na polisi linahusishwa na wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi
Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu
alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango
atoke nje ya nyumba yake.

“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana huenda
wamegongana kwa wanawake ,maana inaonekana marehemu alifungua mlango
akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga
kelele kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.

Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka kama
kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na
mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea
kusiko julikana.

“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa na
kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu
aliamua kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya
kawaida”alisema.

Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti hili kwa
njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi
huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo
ameyasikia.

“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya wanawake mara
nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na majilani,nilipigiwa
simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio hilo,tunaendelea
kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila hata
kuwaeleza sababu”alisema.

Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na
kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa
chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa
zaidi.

Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari
wilayani wilayani hapa Mwang’omba Kegocha(16)amefikishwa katika
mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta(29)

Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali ambapo
mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katikakudaiana wakakorishana ndipo akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment