KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, October 7, 2012

Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima: MJANE WA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI AKANUSHA KUHUSU H...

MJANE WA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI AKANUSHA KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA KATIKA GAZETI LA HABARI LEO


Mjane wa marehemu mwangosi, Aneth ajibu shutuma za kile yaliyoandikwa Katika gazeti la Habari Leo toleo la Tarehe 05/10/2012 kuna habari inayomnukuu mjane wa Marehemu Mwangosi akimlaumu Dkt. Slaa na CDM kuwa ameshindwa kutimiza ahadi yake ya rambirambi na hata msaada wake wa kusomesha mmoja wa mtoto wa Marehemu Mwangosi.
Akizungumza hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja mjini hapa nyumbani kwake asubuhi hii kwa masikitiko makubwa ameshangazwa kuona kile kilichoandikwa katika gazeti la Habari leo na kusema si kweli kwani yale aliyojibu si hayo yaliyoandikwa.
Mjane anaeleza kuwa Dr Slaa hakuahidi rambirambi bali aliahidi kumsomesha mtooto wake wa pili ambaye amemaliza darasa la saba. Ambaye kwa sasa ameanza kupata masomo ya Tuition ambapo msaada huo umetolewa na mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni jirani yake.Mjane wa marehemu ameeleza kuwa kutokana na habari hiyo amekuwa akipata shida sana kwani ndugu zake wamekuwa wakimpigia simu na kumlaumu kutokana na upotoshwaji katika habari hiyo.
Pia amewashukuru wote walioshikiana nae katika msimba wa marehemu mumewe Dadudi Mwangosi na kueleza kuwa ushirikiano ulioneshwa mwanzo wazidi kuonesha.
Mbunge Msigwa akihojiwa ameeeza "kuwa njaa ya siku moja isimfanye mwanahabari yeyote kuvunja maadili na kuandika habari zinazopotosha na kuleta madhara kwa jamii" na kuwataka wanahabari wote kuzingatia maadili yao ya kazi ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii.

NINI UFUMBUZI WA KIFO CHA MAREHEMU DAUDI MWANGOSO

Kuhusu swala la Marehemu Daudi Mwangosi lisilete mtafaruku kwa jamii. Ahadi zilizo tolewa wakati wa Msiba wa Marehemu Mwangosi ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu kama mtu alidanganya hiyo ni nafisi yake nasiyo Matakwa ya wafiwa ni Vizuri kuendesha maombi ya kuitaka Roho ya Marehemu Mwangosi istarehe kwa amani mbinguni.
Kingine ni kuhakikisha UTPC na MCT Waandae mpango wakuweza kuihudumia familiya ya Marehehu mwangosi kielimu na kimaisha, Ikiwa utaandikwa Mradi wenye kuonyesha kusaidia Familia ya Marehemu Daudi Mwangosi hakuna Mfadhili atakaye Kataa, Ifike wakati vyama vya waandishi wa habari vichukue majukumu badala ya kuwa tegemea wana siasa.
Tukikubali misaada ya wanasiasa kila wakati hukoni kununuliwa

By Mkongwe wa Habari Kutoka Songea Mkoani Ruvuma

No comments:

Post a Comment