KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, August 24, 2011

MAISHA YA ADAMU MZUZA NINDI
Ndugu zangu ni vizuri kwanza kujua nani una zungumza naye pili ana pendelea nini.
Kwa jina naitwa Adamu Mzuza Nindi, nilizaliwa 7/7/1954 katika kijiji cha Chiulu wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Elimu ya shule ya msingi nilianza nikiwa na miaka 7 katika shule ya msingi Gatoma nchini Zimbabwe ambako wazazi waliamu kwenda kufanya kazi katika machimbo ya Gatoma Mine Zimbabwe,

Nikiwa Zimbwabwe nilisoma hadi darasa la nne wazazi walipo amua kurudi Tanganyika ,baada ya kufika Tanganyika wakati huo mwaka 1960 nilirudia darasa la kwanza katika shule ya msingi chiulu liyoko Tarafa ya Mbambababay Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma nili rudia darasa ili nielewe lugha ya kiswahili, Nilianza maisha mapya katika kijiji cha Zoole kata ya Chiulu Tarafa mbambabay wilaya ya mbinga mkoa wa Ruvuma

jambo ambalo sita lisahau katika maisha yangu nipale tulipo tayarishiwa chaku wageni kuku alichinjwa na ugali ukawekwa mezani nili jaribu kukata ugali nilishindwa nikamuliza baba kwanini huku wana kula gundi ngumu baba alicheka akasema huu ni ugali wa mhogo ili chukua muda kuuzoea,

kitu kilicho nifurahisha baada ya kufika Tanganyika ili kuwa kupatikana kiurahisi kwa matunda aina ya ndizi tukiwa zimbabwe ndizi tuliziona tukilazwa hosipitali.

Nilisoma katika shule ya msingi chiulu baadaye nilihama kwenda kusoma shule ya msingi Nyoni Mbinga baada ya kufaulu darasa la nne na kuchukuliwa na dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo alikuwa mwalimu wa shule ya msingi nyoni kilometa 40 kutoka kijiji cha chiulu wilaya ya mbinga.

Nikiwa darasa la tano nilihama kwenda kusoma wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa na kujiunga na shule ya msingi Mdete nikiwa dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo aliolewa na na Oddo Matembo ambaye alikuwa ana fanyia idara ya kazi Wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa.

Nikiwa darsa la sita nilihama tena na kwenda kusoma shule ya msingi Wangingombe katika wilaya iringa nilisoma kwa mdu wa miezi sita hatimaye kurudi tena shule ya msingi mdete hadi nilipo maliza shule ya msingi mwaka 1967.

Wakati nikingoja majibu ya mtihani wamatokeo ya darasa la nane dada yangu Alice Nindi aliamua kunipeleka shule ya kulipia mkoani Dodoma ijulikanayo kwa jina la Y.P.Insitute Ovada ambayo ili kuwa iki milikiwa na Father super .

Nilijiunga na secondary ya ovada 1968 na kumaliza masomo yangu mwaka 1972 nilijihusisha na maswala ya biasha kwa kufanya biashara kati ya Tanzania ,Malawi.Zambia,Zimbabwe, Msumbiji, Mpaka Africa kusini. Katika biashara zangu kwa asilimia kubwa likuwa na Tembea kwa mguu pale ilipo bidi biashara za Mkononi hatimaye nafaka mbalimbali.

Mwaka 1974 ili jiunga kuandikia gazeti la Watu ambalo lilikuwa likichapishwa Dar –es –Salaam nilifanya kwa mwka mmoja na kujiunga na Gazeti la Sani nako sikudumu nikajiunga na Gazeti la Mwenge la dini linalo chapishwa Peramiho Songea kipindi chote hicho lilikuwa nikijiendeleza na masomo ya uandishi wa habari,

Mwaka 1980 nilichukua masomo ya dini ya kiislamu na kuweza kufaulu vizuri nilianza kufanya mahubiri katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia, na kuweza kufungua misikiti zaidi ya 5

Mwaka 1985 nililijiunga na Televisheni CNN ambayo makao yake yalikuwa Dar –es – Salaam nime fanyia Tv hiyo kwa muda wa miaka 4 na mwaka 1989 lianza kutuma habari Radio Free Africa na badaye kuanzishwa tv ambako niko mpaka sasa. napenda kuwa fahamisha elimu niliyo pitia na vyeti nilivyo pata na ambatisha hapa chini.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma wakijadili swala la elimu katika shule za msingi na shule za sekondary kuhusu utumiaji wa ligha ya kingereza, kutoka kushoto Juma Nyumayo na katikati ni Adamu Nindi kutoka kulia ni mdau wa Elimu dada Mbogoro

Katibu wa chama cha wandishi wa Habari Andrew Chatwanga na mjumbe wa NCCR Mageuzi ndugu Peter


ADAMU NINDI –ELIMU –SONGEA

Mkuu wa mkoa wa ruvuma Dr Cristina Ishengoma amesema ili kujenga uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne katika somo la kingereza wanafunzi wanatakiwa kusoma somo hilo toka shule ya awali.

Mkuu wa mkoa amesema hayo wakati akihojiana na star tv kwa nini watoto wa shele za sekondari wana shindwa kumudu somo la kingereza.

Wanafunzi wa shule ya secondary ya wavulana songea wamesema katika kuboresha lugha ya kingereza na somo la kingereza ina takiwa kuwa na walimu wenye wito.
,
Nao wanafunzi wa shule ya wasichana songea wamesema msingi wa somo la kingereza ujengwe toka shule za awali .

Inginia haruna makule ,afisa elimu secondary Justin mwingira mwalimu wa shule ya secondary beroya joseph matiko, meneja wa bima mkoa wa ruvuma moses senje wamesema walimu wanao ajiriwa wawe na ujuzizi wa somo la klingereza pia waajibike wajue wapo kazini kufundisha,

Mkuu wa mkoa cristina ishengoma amesema somo la kingereza lianzie shule ya awali na katika bunge lililo pita ili gusia kuhusu kupandisha kiwango cha elimu kwa somo la kingereza
Miongoni ya mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana miongoni mwake ni mkoa wa ruvuma, mkoa umejipanga kukabiliana na swala hilo.

No comments:

Post a Comment