KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, July 26, 2012

MGANGA MASHUHURI WA JADI FROLA NDEMBO AMEPIGWA NA MAJAMBAZI KWA SABABU YA KUSHINDWA KUFANYA UHALIFU

Adam Nindi, Songea

Mganga Maarufu wa Jadi Mkoani Ruvuma Frola Ndembo amenusurika kuuwawa na watu wanaotuhumiwa kuwa ni Majambazi.

Kamanda wa Police Mkoani Ruvuma Deusdediti Nsimike amesema Mganga huyo wa Jadi mwenye Makao yake Namabengo wilayani Namtumbo ambaye Kambi yake hupokea watu 700 na wakulazwa 4o0, usiku wa jana alivamiwa na Majambazi walio dai kuwa anazuia kazi zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma amesema Frola Ndembo alivamiwa majira ya saa 6:00 usiku hatimaye kumteka na kumpeleka porini ambako walimfunga kamba na kumpiga huku wakimwamurisha kuwa aachane na uganga kwa kuwa anazuia kazi za watu.

Wagonjwa waliokuwa kwenye Kambi waliposikia kutekwa kwa mganga Frola Ndembo walisambaa katika vichaka na kumkuta amefungwa kamba huku damu zikimtoka mdomoni na puani kutokana na kipigo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdediti Nsimeki amesema anafanya msako mkali ili kuwabaini wale wote waliousika na swala hilo.

Kamanda wa Polisi Deusdedit Nsimeki ameomba watu wenye taarifa kuhusu watuhumiwa hao watoe taarifa Polisi.

Mganga Frola Ndembo amelazwa Hospitalini mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment