KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, September 6, 2011

Mh Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete akiwa wilayani Mbinga
















KANISA LA THE DOVE QUTREACH CENTER LA USA LA TAKA KUCHOMA KURANI TUJUFU
Ndugu zangu Wakristo na wale ambao hawana Dini.mimi kwa jina nait wa Adamu Mzuza Nindi napenda sana kusoma na kuheshimu mawazo ya kila mtu, jambo la kushangaza ni moja ya machapisho yaliyo tolewa huko Marekani kwa kudai kuwa ifikapo tarehe 11Sepember kanisa lijulikanalo kwa jina la wainjilis wa kikristo kanisa la USA [THE DOVE QUTREACH CENTER] lina jianda kuchoma moto Kurani Tukufu ikitaja kuwa Islaam ni Dini ya Kishetani. [Mungu apishilie mbali mawazo hayo]

Kwanza hiyo dini ijue kuwa Mtu anapo tumia jina la Kiislam siyo maana kuwa Dini ndiyo iliyo mtuma Mtu fanye maovu la ,kila Mtu ana wajibika na lile analo tenda. Kumbukani Yesu Kristo akiwa msalabani mmoja wawana funzi wake alimkata Sikio Myahudi mmoja lakini Yesu Kristo alisema rudisha hilo Sikio ulilo likata .Yesu alijua kuwa yule mtu ametenda kwa kushurutishwa na Shetani jee hawa wakikristo Marekani wange kuwepo wakati huo wange fanyeje . Wailio fanya Maangamizi 11September kwa kushambulia Balozi za Marekani walikuwa hawana utu wa Kibinadamu.

Wako waungwana katika Uislam na wako waungwana katika Ukristo. Mungu alipo kuwa akiumba ulimwengu alisema na tumfanye Mtu kwa mfano wetu [Bibilia] Kurani inasema wanakuuliza kuhusu Roho sema hatukupewa Elimu isipo kuwa kidogo , hiyo inaonyesha kuwa Mtu huwezi kujua kiundani tabia ya Mtu.

Isitumike Dini kwa kufanya maangamizi, jamani kwanza tuna takiwa kulaani kitendo cha kutaka kuchoma Moto KURANI kina takiwa kilaaniwe na watu wanao penda amani. Ni juu ya kila mmoja kulinda heshima za Dini iwe ukrito au uislamu. Watu walio wengi hupenda kuzima Moto kuliko kutafuta chanzo cha Moto.

Ukiangalia idadi ya wakristo ina kadiliwa kuwa Bilioni 2 Duniani kote pia nao Waislamu wapo idadi ya Bilioni Mbili na kitu. Sasa ikifikia hatua ya kuchoma Moto Kurani ni sawa na kutangaza vita kati ya Waislamu na Wakristo. Dini ya Wakristo iliyoko Marekani ni nchi moja wapo inayo tawaliwa na kiongozi shupavu Mh.Obama sasa kuendeleza kusikiliza swala la kuchoma vitabu vya mwenyezi Mungu ni kutangaza hali ya hatari miongoni mwa Dini hizi mbili.

Nimategemeo yangu kuwa Mtu anapo ingia Dini yoyote ile shabaha ya kwanza ni kuleta amani. Naomba wana ulimwengu huu wa Sayansi na Tecolonojia kuliangalia kiundani jambo hili. Kumwingilia Mwenyezi Mungu nikutaka laana, Adhabu ya UKIMWI hatuja maliza, vita kati ya nchi na Nchi nayo ina tukabili. Naomba jambo hili tuli angalie na kuchangia mawazo yetu kwa kina

wenu mpenda amani Adam Mzuza Nindi kutoka Songea Ruvuma Tanzania

No comments:

Post a Comment