KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, September 25, 2011

WAZIRI WA HABARI AWATAKA WAANDISHI KUWA WAADILIFU

Waziri wa Habari utamaduniVijana na Michezo Dr Emanuel John Nchimbi amewataka wana habari kuandika habari zenye uhakika badala ya kutegemea habari za kuandikiwa na bila uchunguzi wowote kuzipeleka katika vyombo vyao vya Habari,Habari ambazo hazija chunguzwa zinazo lenga kuzalilisha viongozi.

Dr Emanuel John Nchimbi amesema hayo baadaya vyombo vya habari nchini kuandika habari za uongo zikidai kuwa Mh. Dr Emanuel John Nchimbi alikimbia na sanduku lenye kura za matokeo ya udiwani katika uchaguguzi wakumtafuta Meya wa Mnspaa ya Songea baada ya aliye Meya wa Mwanzo Ally Saidi Manya kufariki 29/09/2011

Baada ya Uchaguzi kufanyika Chares Mhagama alipata kura 14 dhidi ya kura 12 zilizo mkataa baadaya ya matokeo kutangazwa na Meya kushika nafasi yake ndipo baadhi ya Madiwani walipo leta hoja ya kudai kuwa kura ziliibiwa . Dr Nchimbi amesema kila mtu alikuwa macho na kila kitu kilicho kuwa kikiendelea vipi kura ziibiwe . ,

Dr Emanuel John Nchimbi ameyataka Magazeti yaliyo andika habari hizo za uongo wakanushe habari hizo mara moja kwa kuandika ukurasa wa mbele. Ame ya taka Magazeti ya Majira, Mwanachi na Tanzania Daima kukanusha habari walizo zichapisha mara moja

Mh.Dr Nchimbi amewataka waandishi kutenda haki kama wana weza kumsingizia Waziri wa habari mwenye dhamana katika widhara walioko waandishi jee Mwananchi wa kawaida wana weza kumtendea haki.
kazi kubwa ya waandishi ni kuamusha chachu ya maendeleo katika maeneo waliyoko nasiyo kuandika habari za uongo zenye lengo la kufedhehesha viongozi wao ,

Dr Emanuel John Nchimbi amesema wandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma wanatakiwa wawe mfano wa uandishi wengine Nchini kwa kuandika habari zenye kujenga na kuonyesha njia ya kuya fikia maendeleo .

waziri wahabari Dr Emanuel John Nchimbi amesema Rais ameutunukia mkoa wa Ruvuma Kuwa na Waziri kutokana na Mchango Mzuri wanao ufanya wana Ruvuma katika kuleta Maendeleo ni juu ya waandishi kulinda heshima hiyo kwa kuandika habari Mzuri .

No comments:

Post a Comment