KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, September 16, 2011

MASHOGA WAJA JUU KUDAI HAKI ZAO ZA MSINGI

MKURUGENZI WA TGNP AKIELEZEA HAKI ZA MASHOGA KUSHIRIKI TAMASHA LA JINSIA TANZANIAWaandishi wa habari kutoka Tanzani Bara wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi kuwepo kwa uhalali wa mashoga katika Tamasha amesma kushiriki kwao ni ahaki kimsingi wa haki za binadamu




Dakitari aliye zua kizaa zaa baada ya kusema hadharani kuwa biashara ya kutembea kati ya mwanamue na mwaname ni kinyume na haki kiaafya

Otilia Paulinus Subject: vurugu za mashogaTo: otiliapaulinus@yahoo.comDate: Friday, September 16, 2011, 3:40 PM
Na Otilia Paulinus
VURUGU kubwa zimetokea jana katika Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) baada ya mtaalamu wa masuala ya afya Gerald Samuel kuchangia maadhimio ya nini kifanyike juu ya wanaume na wanawake wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile na kutoa ushauri wa vijana hao mashoga kuacha mara moja biashara hiyo.


Tukio hilo ambalo liliwashangaza wengi walio hudhuria tamasha hilo kutoka ndani na hata nje ya nchi lilitokea majira ya saa 10 jioni katika viwanja vya TGNP Mabibo Dar es Salaam wakati wanaharakati hao wakitoa tathimini nini kifanyike baada ya tamasha ikiwa nchi inaelekea miaka 50 ya uhuru huku wanaume na wanawake wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile wakizidi kushamili.


Kutokana na ushauri na mchango wa mtaaluma huyo kwa wanaharakati hao kutaka wasaidie kupiga vita vitendo vya ushoga na vile vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ndipo kundi la mashoga walipo taka kumvamia na kutaka kumpiga kwa madai kuwa wao wanahaki ya kuwa mashoga.


Baada ya mtaalma huyo kutoka jukwaani ndipo watu hao walipoamua kumfukuza kwa lengo la kutaka kumpiga kabla ya kujisaidia mwenyewe kwa kutimua mbio na kuokolewa na wanaharakati hao na kufichwa katika chumba kimojawapo cha ofisi za TGNP Mabibo. Mashoga hao walisema kuwa wamelazimika kutaka kumshughulikia mwanaharakati huyo mtaalma wa afya za binadamu baada ya kuona ushauri wake ukilenga kuwavurugia biashara yao na kwenda kinyume na malengo ya tamasha hilo ambalo lilikuwa likizungumzia haki na usawa kwa wote.

Walisema kuwa uamuzi waliochukua wa kufanya shughuli hiyo ni uamuzi ambao binadamu wengine wamechagua katika kufanya na ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na ndio sasa ya wao kama binadamu wengine wa Taifa hili wamekuwa wakipigania kwa nguvu zote kuona katiba mpya ijayo inatambua shughuli hiyo ya ushoga.


Walisema kuwa wameshangazwa na mtaalma huyo ambaye ni mwanaharakati badala ya kuwasaidia kuwatetea wanaharakati wenzake ili kuona hakuna mwanaharakati anayebaguliwa yeye anatumia jukwaa hilo la haki na usawa katika kuwabagua binadamu wengine.
Akizungumzia sakata hilo mtaalma huyo alisema kuwa tukio hilo ni sehemu ya changamoto mbali mbali ambazo wanaharakati wanaweza kuzipata katika kufanya harakati mbali mbali za kiukombozi na kuwa pamoja na mashoga hao kutaka kumpiga ila bado kitendo cha mwanaume ama mwanamke kufanya mapenzi kinyume na maumbile si sahihi na ni hatari kwa afya yake.

Alisema kuwa upande wa wanaume wamekuwa wakipatwa na madhara mbali mbali kwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile kama ilivyo kwa wanawake wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile ambao wamekuwa wakipata matatizo makubwa wakati wa kujifungua.
Pia alisema kuwa mashoga wapo hatarini kuathirika kisaikolojia kutokana na kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kuongeza kuwa wakati wowote wanaweza kufa kwa ugonjwa wa UKIMWI.


Hata hivyo baadhi ya wanaharakati wameungana na mtaalam huyo kupinga kwa nguvu zote biashara ya ushoga nchini na kuwa pamoja na kuwepo kwa haki na usawa ila hakuna haki ya watanzania kuona vijana wakiendelea kuteseka ama kupoteza maisha kwa kufanya mapenzi kiyume na maumbile .


Hivyo walitaka pamoja na kuwa na katiba mpya ila bado watanzania wanapaswa kuwa makini juu ya nini kiingizwe katika katiba hiyo vinginevyo iwapo watatoa michango pasipo kutazama mbele zaidi kuna uwezekano wa kuliangamiza Taifa.


Hata hivyo mashoga hao walikuwa wanaitaka katiba imabidishe mfumo wa kuwa tetea mashoga hao kwania nao wanahaki ya kufanya kazi hiyo hivyo wameiomba serikali iweke sheria ya kuwa linda na kuwatetea.

No comments:

Post a Comment