KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, September 16, 2011

WANAHARAKATI WALIA NA UTESWAJI WA WATOTO

Mwanaharakati waTGNP kutoka wilaya ya Mbinga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma P Haule akisikitika juu ya watoto kufanyiwa unyama
Mwanaharakati wa TGNP Liliani Liundi akiratibu mipango ya kutetea watoto pamoja na watu walioko pembezoni hasa wanawake

Wanaharakati wamtandao wa Jinsia Tanzania wameiomba serekari kukabiliana na vitendo vya kuwafanyisha kazi watoto walio chini ya miaka 15 na kuwa tendea vitendo vya kinyama.


Wanaharakati hao wameya sema hayo katika tamasha la 10 linalo endelea jijini Dar – es – salaam lenye lengo la kuwakomboa watu wanao ishi pembezoni hasa wanawake na watoto.wana harakati wameiomba serekari kuwa rudisha haraka watoto wote walioko nchi jirani [ msumbiji] kuwa nusuru na vitendo vya kinyama wanavyo fanyiwa huko.


Mwanaharakati wa TGNP Kutoka wilayani Mbinga ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halimashauri ya mbinga Prisca Haule ameomba serekari kufanya juhudi za dhati kuwa rudisha mabinti wote wakitanzania wanao fanyishwa kazi za kinyama katika nchi jirani [Msumbiji ] ili waje kuendelea na masomo

Amesema watoto walioko nchi jirani [Msumbiji] wanafanyiwa vitendo vya kiovu pamopa na kuuza mili yao, kuchaguliwa watu ambao ni watu wazima


Washuhuda waliona mabinti waliwili walio pata bahati ya kurudishwa kutoka nchi jirani ya [Msumbiji ] Liliani Liundi Mtayarishaji wa Mipango Kutoka TGNP na Juma Nyumayo Mratibu wa mtandao wa mkoa wa Ruvuma RUNECISO wamesema baada ya serekari kufanya juhudi na kufanikiwa kuwarudisha wamesema vitendo wanavyo tendewa mabinti nivitendo vya kinyama na vina paswa kulaaniwa

Mwanaharakati wa TGNP ambaye yuko katika kitengo cha ufuatiliaji na mchambuzi wa mambo ya Jinsia Marjone Mbilinyi amesema umefika wakati sasa kutafuta jinsi ya kuepuka ajira kwa watoto na jinsi ya kuweka mipango ya kulea watoto wetu vizuri


Wageni waalikwa kutoka Marekani Ashley Rajaratnam wamesema Tamasha linalo fanyika Tanzania ni njia moja wapo ya kutoa mwanga kuiwezesha jamii kujua haki zao za msingi kwa pande zote mbili pamoja na kujenga misingi bora kwa wanawake na jamii nzima

No comments:

Post a Comment