KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, April 15, 2012

Makamu wa Rais Mh.Mohamed Bilali akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia jenereta wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma , Jee hali hii ya kufungua majenereta ita isha lini ?



Adam Nindi, Songea
Tanzania kila wakati imekuwa katika swala la kukabiliwa na Matatizo ya Umeme.

Jambo hilo lilisababisha mpaka kipenzi cha Watanzania ajihudhulu Uwaziri Mkuu ili kuwa ridhisha Watanzania ni Ushujaa huo hakuna ambaye anaweza kujihudhuru kwa Maslahi ya Watanzania.

Swala la Umeme limekuwa Tatizo kwa Watanzania, Viongozi wamesikika wakisema kuwa tutamaliza Tatizo la Umeme kwa kutumia Nishati ya Gesi.

Tunajua kuwa hayo yote ni Juhudi za kumkomboa Mtanzania, Jee sisi Watanzania hutuna Rasilimali ambazo zinaweza kusaidia kupata Umeme.?

Hebu tuone wenzetu wana pata Umeme kwa kutumia Victorfall sasa sisi hapa Mkoani Ruvuma tuna Maporomoko ya Maji Nakatuta njia ya kwenda Msumbiji Muhukuru Songea Vijijini.

Tuna Madini ya Urenium Namtumbo Mkoani Ruvuma , Pia tuna Makaa ya Mawe yaliyoko Kata ya Rwanda Kijiji cha Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.

Nini kinatufanya tushindwe kutatua Mgogoro wa Tatizo la Umeme ndugu msomaji hapo nimezungumzia mkoa mmoja tu wa Ruvuma baki ya Mikoa mingine 23 iliyobaki.

Watanzani pale tulipo tusiwe na kawaida ya kulaumu bali tuishauri serekari na kupaze sauti zetu ili serekari itafute njia mubadala ya kumaliza swala la umeme kwa kutumia rasilimali tulizo nazo

No comments:

Post a Comment