KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, April 11, 2012

YALIYO TOKEA YAME TOKEA CHA MSINGI TUMWOMBEE DADA LULU APATE AFYA NJEMA MWAMUZI NI MUNGU NDIYE MWENYE KUJUA UKWELI

Hatima ya msanii maarufu wa kike Elizabeth Michael maarufu kama “Lulu” (pichani) anayeshikiliwa Polisi kutokana na kifo cha Msanii Steven Kanumba iko mikoni mwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisema suala la msanii wa huyo kusema ana kesi ya kujibu au la liko mikononi mwa DPP ambaye atatakiwa kulipitia faili lake na kujiridhisha kama ana kesi ya kujibu au la.

“Kumpeleka Mahakamani ni mpaka DPP tutakapomwasilishia jalada ya tuliyoyakusanya na ndiye atakayeamua kama kuna kesi ya kujibu au hakuna” alisema Kamanda Kenyela.

Alisema hadi hivi sasa wanasubiri ripoti ya uchunguzi wa Daktari ambayo hata hivyo hatatolewa kwa vyombo vya habari kwa kuwa huwa ni siri.

“Bado tunasubiri ripoti ya Daktari na upelelezi unaendelea ila ripoti hiyo ni siri, si lazima apelekwe Mahakamani kesho kwa kuwa bado upelelezi.

No comments:

Post a Comment