KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, May 28, 2012

MIDAHALO YA WAFUMBUA MACHO WANANCHI DODOMA

Omana Gouth na Noel Stephen Mpwapwa

Imeelezwa kuwa katika utendaji wa kazi wa Mahakama za Jamahuri waMuungano wa Tanzania haziko huru kama inavyo ainishwa katika Katiba yaJamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa na wajumbe wa mdahalo wa katiba uliofanyikakatika Ukumbi wa ccm Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ulioendeshwa naMtandao wa Asasi za Kiraia NGOMNET Mpwapwa.Akichanngia mada katika mdahalo huo mmoja wa washiriki Bwana JEMSIKAREIMAHA hakimu mfawidhi wa mahakama wa wilaya ya Mpwapwa alisemakatika utendaji wa kazi katika mihimili mitatu ya dola ambayo ni Serikali,Bunge na Mahakama kunaonekana kuwa serikali inakuwa namadaraka makubwa kuzidi mihimili mingine katika utendaji kazi wake kutokana na muhimili mmoja kuutegemea muhimili wa mahakama kwakuwezeshwa kifedha na vitendea kazi.

Aidha Bwana Kareimaha alidai kuwa katika utendaji wa kazi wa kutoamaamuzi ya kimahakama Rais anaweza kutengua hukumu iliyo iliyotolewana hakimu au jaji kwa madaraka aliyokuwa nayo kikatiba kitu alichosema kinaleta utata wa kiutendaji.

Pia akiongezea mchangiaji mwingine bwana Kandido Mnemele mwakilishiwa kundi la walemavu wilayani mpwapwa (shivyawapwa) alisema kuwa katiba hiyo bado haifahamiki kwa wananchi wa vijijini na wala hawaijuyi rangi yake, na imeandikwa bila kuzingatia uhitaji wa makundi maluumkama walemavu wa macho,

kwa kuandika katiba ya maandishi ya nukta nundu.Bi ELLY MAKALA afisa wa Tasisi wa kuzuia na kupamabana na rushwanchini PCCB alisema kuwa watanzania bila kubadilisha mtazamo wa kuwana maadili na kufuata kanuni na sheria za kazi katiba mpya haiwezi kuwa jawabu la matatizo ya watanzania bila ya viongozi kuwawaadilifu.“Hata tusemeje na tutunge sheria nyingi kiasi gani hatuwezi kutatauamatatizo ya watanzania bila kubadilisha mtazamo wa viongozi kuwawaadilifu,

jawabu la matatizo ya watanzani yamo mikononi mwao wenyewe kwa kujenga moyo wa kushiriki,kupanga na kufuatilia mipango ya kimaendeleo na kuwawajibisha viongozi wabadhilifu’’ Alisema bimakala.Akitoa mada katika mdahalo huo mmoja wa wawezeshaji Daktari Sinda HUSSEN SINDA kutoka chuo kikuu cha Dodoma alisema kuwa TANZANIAhaina Dira na dhima juu ya mstakabali wa Taifa juu ya siasa ujamaa nakujitegemea kuwa wanachi hawajui wanafuata siasa ya mlengo wa namnagani,kibepari,kibwenyenye,ua siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Pia walisema kuwa katika katiba itakayo andikwa iweze kumuangali na kumjali mkulima ya hali ya chini juu umilikaji wa ardhi na sera yauwekezaji ijieleze wazi kwa wakulima wa chini ili kupunguza migogoroya wakulima wawekezaji, na wafugaji.

Mratibu wa mtandao wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali wa wilaya ya mpwapwa bwana Noel Stephen alisema kuwa mdahalo huo una lengo lakuongeza uelewa kwa wananchi juu ya katiba kabla ya mchakato wautoaji wa maoni kwenye tume utakapo karibia.

Na alisema kuwa mradi huu umetekelezwa kutokana na ufadhili kutoka The Foundation for civil society juu kuongeza mahusiano wa wananchi na Wabunge wao majimboni.

No comments:

Post a Comment