KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, May 31, 2012

KIKWETE ANA KOSA GANI JAMANI ?













MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE ANA SITAHILI SIFA ZA KUMWAGA -

Adamu Nindi -Songea "

Has Good Sense of Humour"

Watanzania wenzangu, Mara nyingi na msikiliza mheshimiwa, Rais Jakaya Kikwete akiwa hewani!Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!
Hebu tuone alivyo kuwa akitoa Elimu ya kilimo kijijini kwake
Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!Angalizo:Watanzania Wenzangu , tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kuponda tuu, mara moja moja tupongeze yale mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

Sasa ndugu zangu napenda kuwa fahamisha kuwa mwenye macho haambiwi ona mambo alliyo yafanya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni ya kuigwa na ya kujivunia hakuna Rais ambaye mwenye uwezo wakufanya hayo zaidi ya Rais Gadafi ambaye wananchi wake walimsaliti.

Hebu sasa niainishe yale ambayo hata wewe una weza kuya ona na kuweza kuniunga mkono1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha. 2. Dar –es – salaam tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu. 3.Vyombo vya Usafiri kama Magari yameaanza kutumia Gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55% 4. Kujenga Kivuko na daraja kigamboni. 5.

Ujenzi wa Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma 6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5. 7Ujenzi wa Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

8. Ujenzi wa Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza9. Ujenzi wa Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

10.Ujenzi wa Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.eg Mkoa wa Mbeya

11.Kuweza furusa kwa wawekezaji kusambaza gesi kutoka Songas.pamoja na Kurekebisha mkataba wa Songas, uliokuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini. 12.Kuongeza huduma zaq nishati kwa kutoa Mkataba kwa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

13.Ujenzi wa Barabara Dodoma, Manyara lami. 14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

17.Kuongeza Mradi wa kilimo kwa kutumia njia ya Umwagiliaji maji karibu hekari 20,000 zimejengwa na lengo la Serekari ni kufikia Ekari milioni moja.18. Kilimo kwanza mashamba darasa ya meongezeka na mavuno kuwa makubwa mfano mzuri ni kutoka Mkoa wa Ruvuma lengo lili kuwa kuzalisha kilo milioni 300,000 lakini lengo lilivuka hadi kufikia kilo milioni 400 ,000 mavuno kwa ekari.

19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma ,Lwanda Mkoani Ruvuma makaa ambayo yana uwezo wa kutoa MG 400 za Umeme na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400 na Kuweza kuajiri watu 400 na kupunguza tatizo la Ajira.

23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

26. Ujenzi wa barabara za kisasa nane Dar hadi chalin27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

28. Uboreshaji maabara shule za kata ($ 90Milion

29. Idadi ya walimu kwa ajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom Dodoma uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco Iringa elf 2.5, MkwawaIringa elfu 2.5 Tumaini Iringa elfu 2, Open University elfu 20 nk.

32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele Term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.
36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%. Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000. Jee mpaka hapo huoni hakuna lawama kwa Rais wa Jamhuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete

No comments:

Post a Comment