KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, March 21, 2012

KWA NINI KAMPENI ZA UCHAGUZI ZIFANYWE NA WATU WA INJE JEE WALIOPO HAWA WEZI ?

Ndugu Msomaji wa Mtandao huu napenda nirudi Mwaka 1964 wakati tulipo ungana na Serekari Zanzibar tulichagua ngao inayo ashiria serekari ya Tanzania Ngao ina itwa Adamu na Hawa.

Nembo hii inaashiriria Serekari ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Serekari bila katiba haiwezi kwenda .Ndani ya Katiba kuna ibara ambayo inasema kila mtu ana huru wa kutoa mawazo yake na kwenda kokote anako taka bora kama havunji sheria.

Hebu sasa niende kwenye Mada yangu Mahususi, Utamaduni ulio ibuka sasa Tanzania unamnyima mtu kutoa mawazo yake, Kwa mfano mtu ambaye ni kiongozi aliye chaguliwa awe Diwani au Mbunge akifariki tu nafasi ikiwa wazi watu hujitokeza kugombea .

Sasa cha ajabu ni kuwa Mgombea akisha chaguliwa kugombea kupitia CCM au CHADEMA .Badala ya yeye mwenyewe kupiga kampeni badala yake wapiga kampeni hutoka Dar-es- salaam au sehemu nyingine jambo ambalo lina wachanganya mwananchi wa pale na kupata kiongozi ambaye siyo bora kama waliye kuwa wana mtaka wao.

Nikitoa Mfano katika Kata ya Hanga wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wananchi walimchagua Diwani aitwaye Kasimu Ntara ,kwa kuwa alikuwa hana sehemu ya kukaa alienda kukaa kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mageuzi Mwenyekiti ajulikikanaye kwa Jina la Saidi Kupata,

Mwenyekiti alimkaribisha Nyumbani kwake cha ajabu badala ya kusimamia kazi za maendeleoDiwani huyo Kasimu Ntara akaingia katika swala la mpenzi akampa mimba mtoto wa Mwenyekiti Said Kupata ambaye alikuwa kidato cha pili .

Viongozi wa Ngazi za Juu baadala ya kumwajibisha Diwani Kasimu Ntara badala yake Baraza la Madiwani wa kamteua Diwani Kasimu Ntara kuwa Makamu Mwenyekiti mbali ya kufanya kitendo kiovu kwa mtoto wa Mwenyekiti Said Kupata

Sasa hii ina vunja mioyo kwa wananchi Diwani huyu Kasimu Ntara ni wanamna gani kwa nini asiajibike badala yake anaongezwa cheo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani ,jee ana weza kusimamia maendeleo kwa upande wawatoto wa kike .

Kwa ushauri wangu wagombea wangeachwa wenyewe ili wananchi wapate nafasi ya kuwa tafakari kuliko kuleta majeshi kutoka nje siku ya siku viongozi hao wanaishia kuwapa mimba watoto wa viongozi na masikini

No comments:

Post a Comment