KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, March 16, 2012

RAIS ATEUA WA KUU WA MIKOA MIPYA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa mipya minne iliyotangazwa na Serikali hivi karibuni. Katika uteuzi huo uliyotangazwa jana Rais Kikwete amemteua Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI.Wengine walioteuliwa ni Magalula Saidi Magalula anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA, Paschal Kulwa Mabiti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU na Kapt. Asery Msangi anayekwenda kuongoza Mkoa wa Njombe, kabla ya hapo Kapt. Msangi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.Kwa upande wake kabla ya hapo Magalula kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Rutengwe kabla ya uteuzi huo mpya alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda huku Mabiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka mawasiliano Ikulu viongozi wote hao wanatarajiwa kuapishwa Machi 21, 2012 Ikulu jijini Dar es Salaam, saa 04:00 asubuhi na uteuzi huo umeanza tangu jana Machi 15, 2012.

No comments:

Post a Comment