KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 24, 2011

WANAHABARI WAPATWA NA MSIBA RUVUMA

MAREHEMU LEVINA NDUNGURU

Wanahabari wa Mkoa wa Ruvuma wamepatwa na msiba mkubwa kwa kufiwa na mhudumu aliye kuwa akifanya kazi katika ofisi ya Mpenda Mvula ambaye ni mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma,


Mhudumu aliye kufa au kuuwawa ni Levina Ndungu ambaye alikuwa na Umuri wa Miaka 26 .siku ya tukio marehemu akiwa ofisini alikuja kijana aliye julikana kwa jina la Tomas Jirara mwenyeji wa mwanza akidai ana taka kuchapiwa barua yake na kuweza kulipa shilingi mia tano.


Mhudumu Levina Ndunguru bila kujua nia ya kijana Tomas Jirara alichapa barua hiyo na huku kijana huyo Tomas Jirara 22 akionyesha ukarimu wa hali ya juu kwa Levina Ndunguru hatimaye levina ndunguru kuanguka katika Mapenzi jambo ambalo kijana huyo Tomas Jirara 22 alikuwa amelipanga


Mara baada ya kumaliza kazi alimtoa out ingawa haijulikani ni wapi alimpeleka lakini kwa mujibu wa tarifa iliyo tolewa na kaimu kamanda waPolice mkoa wa Ruvuma .Zina sema Marehemu Devina Ndunguru akiwa na kijana Tomas Jirara walirudi saa 1.00 usiku walipewa chumba katika nyumba ya wa geni Mikumi Mfaranyaki , Tomas Jirara aliweza kumua Levina Ndunguru majira ya 8.00 usiku ,lakini alipohojiwa na POLICE ana sema aliweza kufanya kitendo cha kinyama kati ya saa 2.30 usiku au saa 2.45 akinukuriwa anasema mara baada ya kufanya mapenzi na Levina Ndunguru wakiwa kwenye mapenzi walikorofishana ndipo alipo mpiga ngumi moja nzito mwisho kumalizia kumvunja shingo alieleza mbele ya police bila hata kigumimizi.


Tomasi Jirara alipo fanikiwa kumua Levina Ndunguru alimpekua na kuchukua funguo za ofisi inayo milikiwa na Mpenda Mvula na kwenda kufungua na kuiba Comyuta moja ,Printer pamoja na Cheki yenye Thamani ya Shilingi 150,000

Baada ya kukamilisha wizi wake alianza safari kuelekea njia ya Lindi alipo kamatwa na Police, SASA HEBU ANGALIA PICHA YA MUUAJI NA BINTI ALIYE UWAWA HALAFU TOA MAJIBU, TUFANYE NINI NA MABINTI ZETU ?

1 comment:

  1. Hongera sana kwa kazi nzuri, ni vigumu kujua siri nzito iliyo moyoni mwa mtu kwani moyo ni kiza kinene. Cha msingi ni kuwa dada zetu wawe makini sana katika mahusiano yao pia wazazi tuwe waangalifu sana kwa mabinti zetu hususani katika masuala ya mapenzi mana mabinti wengi huwa ukarimu sana katika masuala haya na kutoa dhamana hata kwa mtu wasiomfahamu vizuri.Kitendo hicho kimeniuma sana naomba sheria ichukue mkondo wake na huyo kijana ahojiwe vizuri ili tujue lengo lake mbali na hilo la wizi ofisini kwa marehemu!

    ReplyDelete