KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, May 3, 2013

MACHIMBO YA MAKAA YA MAWE YA NGAKA MKOANI RUVUMA YANA MKOSI GANI ?

 Hapa unapo paona ndiyo sehemu inayo patikana makaa ya mawe eneo la Ngaka, ni eneo ambalo Serikali ili chukua hatua baada ya kuona Makaa yakiungua zaidi ya miaka 4 moto ambao uliigharimu serekali ya Tanzania shilingi milioni 59 kuuzima moto ulio kuwa ukiunguza makaa hayo
 Baada ya kufanikiwa kuuzima Moto ulio kuwa ukiunguza Makaa ya Mawe Viongozi mbalimbali walianza kuwasili eneo la Ngaka kuangalia jinsi ya uchimbaji akiwemo Makamu wa Rais Gharib Mohamed Bilali hapo akisalimiana na wamiliki wa machimbo ya TAN COAL
 Mh. Makamu wa Rais alipo wasili Mkoani Ruvuma ili kukagua miradi mbalimbali ikiwemo machimbo ya Mawe ambayo yameonyesha kuleta ufanisi Mkoani Ruvuma
 Kampuni ya TAN COAL ikiwa kazini kuchimba Makaa ya Mawe na kuweza kuwatia tumaini wakazi wa Ngaka kuona sasa umasikini utawatoka kwa kuajiliwa pia kuweza kuuza bidhaa zao kiurahisi eneo la Machimbo
 Kamati ya Bunge inayo husiana na Viwanda ilipotembelea eneo la Machimbo na kuhakikisha kuwa Wananchi wako shwali na Machimbo hayo, pia ilifanya mkutano na wananchi na wao kudai ajira. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu akiwa mmojawapo  aliye wahi kufika na kuchukua Changamoto za Ajira katika eneo hilo.
 Viongozi waandamizi wa NDC nao waliweza kuhudhulia vikao mbalimbali ambavyo vilikuwa havina migogoro mikubwa, zaidi wana kijiji waliomba huduma muhimu kama Maji, Ajira, Pamoja na wao kupewa kipaumbele kwa mambo Muhimu
 Mmoja wa Maafisa wa TAN COAL ndugu Didi aliweza kuihakikishia Kamati ya bunge juu ya Ajira kuwa atatoa kipaumbele kwa wazawa lakini alitoa angalizo atatoa ajira kutokana na Elimu waliyo kuwa nayo na si vinginevyo
Haya ni makaa yaliyo anzwa kuchimbwa lakini kutokana na Siasa kuingia kila mahali Wananchi wa hapa wamepandikizwa kuhusu fidia waliyo pewa kuwa ni ndogo kiasi cha kuifanya Serekari kuwa na kauli Tata kuhusu swala hilo huku wakijua Makubaliano toka Machimbo hayo yana anza, Jee huu ndio uwekezaji wa kuweza kuwa katisha Tamaa wawekezaji?, Hivi Tuseme Toka Mwanzo juhudi za kudai Fidia zilikuwa wapi?  Watanzania tujifunze kuleta Vurugu eneo la Wachimbaji tuna jikosesha ajira wenyewe
Mbunge wetu Gaudence Kayombo wewe ndiye tuliye Zima Moto wa Makaa ya mawe kwa nini huwezi kueleza ukweli kuhusu hali ilivyokuwa hapo zamani? Jee baada ya kuendeleza hawa wawekezaji ndiyo Vurugu zianze Watanzania siasa za kuzorotesha Maendeleo tuachane nazo, tuwe wakweli wala tusiwe Mashabiki tunapo ona Wawekezaji Wakionewa, Nimeonyesha picha zote na kuonyesha viongozi walio kuja kabla ya kuchimba makaa hayo hao wote walikuwa wapi kujua haki za wananchi zina punjwa? , Watanzania tuwe na soni kwa Mambo mengine.

No comments:

Post a Comment