KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, May 5, 2013

WABUNGE WETU MKOANI RUVUMA UMOJA WENU UPO WAPI KIMAENDELEO

Mh.Stella Manyanya hivi sasa Mheshimiwa Rais alitaka apate jinsi mlivyo tekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mambo mliyo tumwa na CCM katika majimbo yenu. jee Mheshimiwa baki ya kuwainua Wanawake Kiuchumi lipi lingine ulilo litekeleza Blog hii ina taka kuwa julisha wapiga kura wako wa Mkoa wa Ruvuma
 Mheshimiwa Emanuel John Nchimbi Mbunge wa Jimbo la Songea Hatuna ubishi kwa kazi ulizo zifanya,1 . Kuhakikisha kila kata ina Sekondary,2,kuendeleza mji na kuwa Manspaa ya Songea 3.Kujenga sekondaei ya kidato cha tano na sita 4,Manspaa ya Songea hivi sasa ina walao barabara za lami5. Kuimarisha huduma za Afya ,Mwisho kuwa na ushirikiano na vyama vya upinzani katika maendeleo Hongera
 Mheshimiwa Jenista Mhagama 1.Kutoa Pongezi kwako kwa kuweza kutuwakilisha katika Bunge ukiwa Mwenyekiti. Kuteuliwa katika kamati mbalimbali zenye kupigania maendeleo. 3.kuweza kujenga makao makuu ya Halimashauri ya Wilaya Songea Vijijini .lakini la mwisho jaribu kurudisha umoja wenu wawa bunge ili wananchi wapate maendeleo
 Mheshimiwa Kazi unayo, umeapa kwa katiba kuwa utatekeleza ilani ya chama Wananchi wana ngoja Barabara ya Namtumbo - Tunduru kuwa na Lami, Pamoja na kazi ulizo fanya za kuweza kuweka bei nzuri ya Korosho, Wananchi wana ngoja barabara ya Lami.
 Mheshmiwa Vita Kawawa Umenyosha juu ilani ya Chama cha mapinduzi kuleta Maendeleo kwa Wananchi wa Namtumbo, 1. Swala la Barabara umesimamia vilivyo. 2.Juhudi za Kuweka umeme wilaya ya Namtumbo umefanikiwa. Vitu unavyo daiwa Nikuwa na Hospitali ya Wilaya Namtumbo. Pia Uchumi wa Wananchi wa Namtumbo wana Tegemea Tumbaku Simamia Bei ya Tumbaku iwe Nzuri. Mwisho simamia kutoa Mfumo Dume ulio kithiri wilaya ya Namtumbo
 MheshimiwaMtutula Mtutula  na Jua una mambo mengi ya kufanya lakini una jua jinsi ulivyo weza kuwa fanya wananchi wa wilaya ya Tunduru kuwa kitu kimoja, Jambo la Mhimu kwako ni kutokomeza siasa zinazo ingizwa katika Dini ukifanya hilo uchumi wa Tunduru uta kuwa kama ulivyo lenga Mwenyewe
 Cap.John Komba wewe ni Mwamba wa Mashairi Juhudi zako Zimetufanya Mkoa wa Ruvuma Tuishi vizuri na Majirani Msumbiji,Malawi, na Hata Zimbabwe.Tunaomba uliyo fanya Wilaya ya Mbinga basi Hamishia wilaya Mpya ya Nyasa ukiweza Kuijenga Wilaya ya Nyasa kwa Ujasili ulio nao mwaka 2015 ni wako
Mheshimiwa Gaudence Kayombo wewe una jijua kuwa Fani yako ni Uchumi jitahidi achana na Hasira endeleza yale uliyo panga kwa wananchi wako hivi sasa Mbinga ina Umeme ,Barabara za Lami,Pia hata uchumi una zidi kupanda, Watu wasio na Furaha na Maendeleo ndio wanao kukatisha Tamaa, Chukua Moyo wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa na Uvumilivu.Hasira za Mkizi furaha ya Mvuvi.Makaa ya Ngaka yana ngoja Busara zako

No comments:

Post a Comment